18 Julai 2026 - 16:16
Kwa Nini Iran Ililenga Kambi ya Al-Tanf? Ujumbe wa Kisiasa Unaozidi Ewanja wa Vita

Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) wameripotiwa kulenga kambi ya kijeshi ya Marekani ya Al-Tanf, kusini mwa Syria, katika awamu ya 11 ya operesheni ya “Nasr 2”, huku wachambuzi wakisema umuhimu wa shambulizi hilo unaweza kuwa mkubwa zaidi katika ujumbe wake wa kisiasa na kimkakati kuliko matokeo yake ya moja kwa moja ya kijeshi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) wametangaza kulenga kambi ya kijeshi ya Marekani ya Al-Tanf, iliyoko kusini mwa Syria, katika awamu ya 11 ya operesheni ya “Nasr 2”.
 
Ingawa shirika la habari la Reuters, likinukuu chanzo cha kijeshi nchini Syria, limedai kuwa shambulizi hilo halikusababisha uharibifu au vifo, wachambuzi wanaeleza kuwa umuhimu wa tukio hilo unaweza kuonekana zaidi katika ujumbe wake wa kisiasa na kimkakati kuliko matokeo ya moja kwa moja kwenye uwanja wa vita.
 
Kwa mujibu wa gazeti la *Al-Akhbar*, uchaguzi wa kambi ya Al-Tanf unaweza kuwa na maana mbili; kwanza, kuwa ni jibu kwa uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo hilo, na pili, kuwa ni ujumbe usio wa moja kwa moja kwa Damascus, hasa katika kipindi ambacho serikali ya mpito ya Syria imekuwa ikijaribu kubaki katika msimamo wa kutofungamana na upande wowote katika mvutano kati ya Iran na Marekani.
 
Shambulizi hilo pia liliripotiwa kufanyika saa chache baada ya maafisa wa Syria kudai kugundua shehena ya ndege zisizo na rubani (drones). Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa na Hizbullah.
 
Kwa mtazamo wa wachambuzi, kulengwa kwa Al-Tanf kunaweza kuashiria kuwa operesheni hiyo haikulenga tu kutoa jibu la kijeshi, bali pia kutuma ujumbe mpana kuhusu uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo hilo na mabadiliko ya mienendo ya kisiasa na kiusalama nchini Syria.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha